Nabii Natasha wa Kenya Alivyopokelewa kwa Shagwe Bongo – Video

Nabii Lucy Natasha, kutoka nchini Kenya, ametua nchini usiku wa Julai 03, na kupokelewa kwa shangwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Nabii Natasha amekuja nchini kwa ajili ya mkutano wa kiroho atakaoufanya kwa kushirikiana na Nabii Peter Nyaga. Mkutano huo ulianza tangu Julai 1, na utamalizika Julai 7, mwaka huu katika viwanja vya Tabata Liwiti jijini Dar.

Watu kutoka dini zote, madhehebu yote, wanakaribishwa kwa ajili ya kufunguliwa, kuombewa matatizo yao, wenye maradhi, waliokata tamaa wote wafike ili waweze kufunguliwa na kukabidhiwa mikononi mwa Yesu Kristo.

Aidha mkutano huo utapambwa na burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali wa injili akiwemo, Emmanuel Mbasha, Christina Shusho na wengine.

TAZAMA VIDEO HII

Loading...

Toa comment