NABII OLIVIA, ELISHA WATIMIZA MWAKA MMOJA WA HUDUMA
MWANAMUZIKI wa nyimbo za injili, Upendo Nkone, amewapongeza Nabii Olivia na mume wake Elisha Mtangirwa kwa kutimiza mwaka mmoja wakitoa huduma ya neno la Mungu ndani ya kanisa lao.
Aidha Upendo Nkone ametoa ushauri kwa watu wote waliokata tamaa kwa kuzidiwa na matatizo ya kila aina kukimbilia kwa Yesu Kristo ili waweze kuondokana na matatizo yanayowasumbua pia kuhudhuria kanisani kadri wawezavyo.
Nabii Olivia na Mtume Elisha wametimiza mwaka mmoja ya utoaji huduma ya kiroho ya kumtumikia Mungu na wamewaomba watumishi wao waendelee kuwapa ushirikiano kutokana na huduma wanayoitoa.
Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili walikuwepo wakiongozwa na Upendo Nkone.
Comments are closed.