The House of Favourite Newspapers
gunners X

NACTE Yafuta Matokeo ya Mtihani wa Diploma ya Utabibu

0

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limeifuta matokeo ya mitihani ya Dimploma (NTA-Level 5) ya Utabibu iliofanyika kati ya Agosti 12 na Septemba 11, mwaka huu ambapo mitihani hiyo na mwongozo wa kusahihisha mitihani hiyo inadaiwa ilivuja katika vyuo 147 nchini.

 

Inadaiwa kwamba mitihani hiyo ilivuja kupitia mamlaka zilizopo chini ya Wizara ya Afya na zikishirikiana na baadhi ya vyuo kisha wanafunzi kutumiana mitihani hiyo pamoja na mwongozo wa usahihishaji katika mitandao ya kijamii hasa Telegram na WhatsApp.

 

Oktoba 15, Wizara ya Afya iliwaandikia barua wakuu wote wa vyuo vyenye zaidi ya wanafunzi 4,000 ikieleza imepokea barua kutoka Nacte ikieleza matokeo yote ya wanafunzi wa clinical medicine (uganga) yamazuiwa.

 

Barua hiyo ya Nacte iliyoandikwa Oktoba 12, ina kumbukumbu CA.64/170/01B/7 inayohusu kutolewa kwa matokeo ya awali (provisional results) ya mitihani iliyofanyika kitaifa Agosti katika vyuo vyote vya kati vya afya.

 

“Baraza linapenda kuwafahamisha kuwa matokeo yote ya wanafunzi wa ngazi ya NTA level 5, program ya utabibu yamezuiwa mpaka taarifa ya uchunguzi kutoka Wizara ya Afya itakapokamilisha na kuwasilishwa Nacte kwa ajili ya maamuzi,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

 

Barua hiyo imeeleza kuwa “Matokeo ya wanafunzi 35 kutoka vyuo mbalimbali yamefutwa na wanafunzi hao kusimamishwa kuendelea na masomo (discontinued) kutokana na kufanya udanganyifu kwenye mitihani.

Leave A Reply