The House of Favourite Newspapers

Nado Aongeza Mkataba Mpya Azam Fc

0

Kiungo mshambuliaji wetu, Idd Seleman ‘Nado’, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex.

Nado amesaini mkataba huo leo Jumanne mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.


Nyota huyo amekuwa na kiwango tokea msimu uliopita alipojiunga nasi akitokea Mbeya City, hadi sasa msimu huu akiwa amehusika kwenye mabao 12 ya Azam FC, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.

Leave A Reply