The House of Favourite Newspapers

Nafasi Ya Kazi Kwa Software Developer

0

Global Publishers & General Enterprises LTD, kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi na Amani, na wamiliki wa mitandao, Application na Platforms za internet mbalimbali, ina nafasi ya kazi ya Developer/Programmer, mwenye elimu na sifa zifuatazo:

ELIMU:

Anahitajika kijana wa kiume mwenye Shahada ya Sayansi ya Kompyuta (Bachelor of Computer Science) au Diploma ya Kompyuta Sayansi.

SIFA:

Aidha, mtarajiwa awe kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 25, anayeishi jijini Dar es Salaam, muaminifu, mchapa kazi mwenye uelewa wa kutosha wa masuala ya Web na Mobile Applications Development, Programming and Maintenance. Awe na ujuzi wa kufanya kazi hizi usiopungua miaka mitatu (3) katika kampuni inayotambulika na mwenye uwezo wa kusimamia na kuendesha Applications na Platform mbalimbali. Awe tayari kufanya kazi kwa kujituma bila kusimamiwa na mwenye uwezo wa kujifunza na kuelewa teknolojia mpya.

Mwisho:

Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuletee ofisini barua yako ya maombi ya kazi haraka, iliyoambatana na CV yako pamoja na vivuli vya vyeti vyako, kwa:

MENEJA MKUU

S.L.P 7534

DAR ES SALAAM

Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Bamaga (Nyuma ya TSN Petrol Station na Supermarket).

Simu: 0715 288627.

Mwisho wa kupokea maombi ni Septemba 15, 2017.

Leave A Reply