Nafasi ya Kazi, Mtafutaji wa Matangazo

Global Publishers Limited, inatafuta kijana mwenye uzoefu wa kutafuta matangazo kwa ajili ya magazeti, tovuti na mitandao mingine ya kijamii.

Kama wewe unao uzoefu mkubwa na umeshafanya kazi hii katika vyombo mbalimbali vya habari, lakini kwa sasa huna kazi, tafadhali njoo ofisini kwetu HARAKA ukiwa na Barua na Cv yako mkononi.

Mwenye sifa na vigezo atalipwa mshahara pamoja na kamisheni nzuri kwa kila tangazo atakalolipata.

Mwisho wa kupokea maombi ni Aprili 22, 2017

Maelezo yako elekeza kwa:

MENEJA MKUU S.L.P 7534

Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu,

Sinza Bamaga (Nyuma ya TSN Petrol Station).

Simu: 022 2773356 au 0715 288 627

 

Loading...

Toa comment