The House of Favourite Newspapers

Nafasi Ya Kazi Mwandaaji Mkuu Wa Maudhui Ya Televisheni Ya Mtandaoni

 

GLOBAL TV ONLINE ni televisheni ya mtandaoni iliyo na makao makuu yake jijini DAR ES SALAAM, TANZANIA ikiwa na watazamaji dunia nzima zaidi ya milioni ishirini kwa wiki na watazamaji waliojisajili zaidiya milioni moja na laki nane. Kama sehemu ya mafanikio yake Global Tv Online inatafuta mbobezi wa uandaaji wa maudhui ya mtandaoni hasa mwenye uelewa wa juu kwenye maudhui ya You Tube.

 

MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa maudhui, kufanya utafiti, kufuatilia habari na kuzipakia kwenye mtandao waGLOBAL TV ONLINE kwa wakati pamoja na kusimamia kazi hizo kwa watendaji walio chini yako. Katika kutimiza hilo GLOBAL TV ONLINE itajikita katika kutoa habari za kweli na zenye viwango vya kimataifa.

 

MALENGO YA KAZI JOB PURPOSE

Kuwa wa kwanza katika kutoa habari za papo kwa papo na za kipekee. Kuwajua washindani wako na namna bora ya ushindani. Kuwa na uelewa wa hali ya juu kuhusu ubora wa video.

 

MAJUKUMU MAHUSUSI

Kuongoza timu ya GLOBAL TV, kuunganisha nguvu katika kutafuta habari, kuripoti habari, kufuatilia matukio na kuandaa maudhui zenye nguvu na za kuvutia. Hili litapimwa kwa mwitikio wa watazamaji kwa siku na kila mwezi.

 

UJUZI

Awe anajua kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza vizuri. Awe na historia ya kusimamia na kuongoza mitandao ya You Tube yenye nguvu na maudhui bora. Awe na historia ya kuandaa maudhui zenye ubora zaYou Tube.

 

WELEDI

Awe na uwezo wa kufikiri haraka na mwenye uwezo mkubwa wa kutafsiri mawazo kwenda kwenye uhalisia. Awe na uwezo wa kupata suluhisho na kutatua changamoto kwa haraka.Awe ma uwezo wa kuona bali na kuzipatia majibu ya haraka changamoto kwa ajili yake na timu. Awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yoyote na kubadilika kwa haraka kutokana na mazingira.

KAMA UNADHANI UNAZO HIZO SIFA TAFADHALI TUMA CV YAKO NA UWE TAYARI KWA AJILI YA USAILI KABLA YA TAREHE 25 NOVEMBER.

KWA MENEJA MKUU 

MWANDAAJI MKUU WA MAUDHUI WA GLOBAL TV

GLOBAL GROUP

SINZA MORI

DAR ES SALAAM

SIMU: 0754 290 167

Comments are closed.