The House of Favourite Newspapers

Nafasi Ya Kazi: Ofisa Masoko Dar, Mwisho wa Kutuma Maombi Juni 15, 2025

Global Publishers Ltd, wamiliki wa Global TV Online na mitandao yake ya kijamii, inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya Ofisa Masoko.

🔹 Sifa Muhimu:

  • Uzoefu usiopungua miaka 2 katika kutafuta masoko na matangazo kwa vyombo vya habari.
  • Uwezo wa kuandika na kuwasilisha mapendekezo ya kibiashara (Proposals) kwa weledi.
  • Uwezo wa kuzungumza na kuandika kwa ufasaha Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe mkazi wa Dar es Salaam na anayefahamu mazingira ya biashara ya vyombo vya habari.
  • Uwezo wa kufanya kazi kwa mfumo wa retainership na commission-based (kwa malipo ya msingi na ya tija).

🔹 Tunatafuta mtu mwenye:

  • Ushawishi na uelewa wa masoko ya kidigitali na matangazo ya biashara.
  • Uwezo wa kujenga mahusiano ya kibiashara na wateja wa sekta mbalimbali.
  • Nidhamu ya kazi na ufuatiliaji wa malengo ya kimauzo.

🕔 Mwisho wa kutuma maombi: Juni 15, 2025.

📩 Tuma wasifu (CV) wako pamoja na barua ya maombi kupitia:
📧 WhatsApp: +255 789 515432

Au leta moja kwa moja katika ofisi zetu: Global Publishers Ltd, Sinza – Mori, Dar es Salaam.

Fursa hii ni kwa wale walio tayari kufanya kazi kwa matokeo. Jiongeze!
#Ajira #MarketingJob #GlobalTVOnline #Careers #OfisaMasoko