NAFASI YA KAZI RECEPTIONIST, GLOBAL GROUP DAR

Global Group, kampuni mama ya Global Publishers, kampuni inayomiliki vyombo vya habari vya magazeti, televisheni na redio ina nafasi ya kazi ya RECEPTIONIST, mwenye elimu na sifa zifuatazo:

ELIMU:

Anahitajika RECEPTIONIST mwenye Elimu ya A Level au Chuo Kikuu na mwenye ujuzi wa kutumia kompyuta na programu zote za kiofisi.

Awe na uwezo wa kuongea na kuandika kwa UFASAHA, lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

SIFA:

Aidha, mtarajiwa awe kijana wa kike mwenye umri wa kati ya miaka 25 – 30, anayeishi jijini Dar es Salaam eneo la SINZA, MWENGE au KINONDONI, muaminifu, mchapa kazi mwenye uelewa wa kutosha wa masuala ya utawala wa kiofisi. Awe ameshawahi kufanya kazi za kiofisi katika kampuni yoyote kwa muda usiopungua mwaka mmoja.

 

Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuletee ofisini barua yako ya maombi ya kazi haraka, iliyoambatana na CV yako pamoja na vivuli vya vyeti vyako, kwa:

MENEJA MKUU

S.L.P 7534

DAR ES SALAAM

Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Mori (Global Group, zamani

Johannesburg Hotel). Simu: 0715 288627. Mwisho wa kupokea

maombi ni JULAI 30, 2019.


Loading...

Toa comment