Nafasi Za Ajira Za Mikataba 400 Kwa Kada Za Afya, Mwisho wa maombi Desemba 20, 2024
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya inaendelea na utekelezaji wa mpango wa uwekezaji katika afya ya mama na mtoto nchini Tanzania yaani Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCHIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye uwezo na sifa za kujaza nafasi za ajira za 400 za Mkataba kwa Kada za Afya watakaofanya kazi katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini.
Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 6 – 20, Desemba, 2024. Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).