Nafasi za Kazi 1,596 TRA Kada Mbalimbali, Mwisho wa maombi ni leo Feb 19
TRA inapenda kuajiri watumishi wenye sifa, uwezo na maadili kushika nafasi za kazi katika Idara ya Mapato ya Ndani, Forodha na Ushuru, Usimamizi na Utawala wa Rasilimali Watu, Huduma za Sheria, Menejimenti ya Manunuzi, Utafiti na Mipango, Fedha, Ukaguzi wa Ndani, Mambo ya Ndani na Idara ya Vihatarishi na Uzingatiaji. Kwa hiyo maombi yanaalikwa kutoka kwa Watanzania wenye sifa, imeeleza taarifa hiyo.
Nafasi hizo zipo katika kada zifuatazo: Ofisa Msimamizi Ushuru daraja la II (573), Ofisa Forodha daraja la II (232), Msaidizi wa Usimamizi wa Ushuru daraja la II (253), Msaidizi wa Forodha daraja la II (154), Mhadhiri Msaidizi (15).
Nyingine ni: Ofisa Usimamizi Data daraja la II (20), Ofisa Rasilimali Watu daraja la II (11), Ofisa Utawala daraja la II (3), Ofisa Usafirishaji daraja la II (5) na Ofisa Milki daraja la II (15).
Pia TRA imetangaza nafasi za: Wahandisi daraja la II (12), Wajiolojia daraja la II (2), Ofisa Hesabu daraja la II (12), Mhasibu daraja la II (2), Ofisa Mambo ya Ndani daraja la II (10), Ofisa vihatarishi daraja la II (8) na Wachumi daraja la II (6).
Nafasi nyingine zilizotangazwa ni pamoja na: Watakwimu daraja la II (4), Mwanasheria daraja la II (6), Ofisa Manunuzi na Usambazaji daraja la II (5), Ofisa Maabara (3), Mkutubi daraja la II (4), Ofisa Taaluma daraja la II (2).
Mkaguzi wa Ndani daraja la II (2), Mlinzi daraja la II (2), Ofisa Uhusiano daraja la II (5), Msaidizi wa Mafunzo (2), Katibu Muhtasi daraja la II (12), Mtaalamu wa Maabara daraja la II (4), Ofisa Hesabu Msaidizi (10), Msaidizi wa usimamizi wa rekodi daraja la II (10).
Nafasi nyingine ni: Mafundi uashi na umeme daraja la II (10), Mwendesha mfumo wa ulinzi daraja la II (9), Nahodha daraja la II (8), Fundi boti (8), Mkutubi msaidizi daraja la II (2), Nahodha msaidizi daraja la II (2), Mtu wa mapokezi daraja la II (20), Dereva daraja la II (105) na Msaidizi wa ofisi daraja la II (27).
BONYEZA HAPA KUSOMA >>> TANGAZO LA KAZI TRA
Mwisho wa kutuma maombi ni Februari 19, 2025