Nafasi Za Kazi 3633 Za Ualimu, Mwisho wa Kutuma Maombi Desemba 20, 2024
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi elfu tatu mia sita thelathini na tatu (3633) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
MWALIMU DARAJA LA III C – SOMO LA BIASHARA (BUSINESS STUDIES)
NAFASI 3425
Mkoa – Arusha 102, Dar Es Salaam 14, Pwani 107, Dodoma 180, Geita 150, Iringa 103, Kagera 190, Katavi 63, Kigoma 154, Kilimanjaro 135, Lindi 131, Manyara 135, Mara 205, Mbeya 149, Morogoro 153, Mtwara 136, Mwanza 163, Njombe 85, Rukwa 67, Ruvuma 154, Shinyanga 113, Simiyu 143, Singida 126, Songwe 98, Tabora 163, Na Tanga 206.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Desemba, 2024