Nafasi za Kazi; Anahitajika Afisa Masoko Mwenye Uzoefu
GLOBAL PUBLISHERS AND GENERAL ENTERPRISES LIMITED; Wamiliki wa Global TV, Global Radio na mitandao yake ya kijamii inayofuatiliwa na watu wengi ndani na nje ya nchi inatangaza nafasi ya kazi ya AFISA MASOKO mwenye uzoefu wa kutafuta masoko kwenye vyombo vya habari (utafutaji wa matangazo) wenye ujuzi na sifa zifuatazo;
SIFA:
– Awe na Elimu ya Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates ya Biashara au Ugavi.
– Awe mwenye kujiamini na mwenye uwezo wa kumshawishi mteja.
-Awe na uzoefu wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiswahili na Kingereza na awe anaishi jijini Dar es Salaam.
Pia tunakaribisha maombi ya watu wenye uzoefu na masuala ya matangazo kuomba kama FREELANCERS ndani na nje ya Dar es Salaam.
Mwisho:
Kama unakidhi vigezo vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuletee barua yako ya maombi ya kazi haraka ofisini iliyoambatana na CV yako pamoja na vivuli vya vyeti vyako, kwa:
MENEJA MKUU,
S.L.P 7534,
DAR ES SALAAM
Au wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Mori (Global Group House).
Email: [email protected].
Mwisho wa kupokea maombi ni Julai 31, 2024.