Nafasi za Masomo Kidato cha 5, Shule Sekondari Msangani, Kibaha

Shule ya Sekondari Msangani yenye namba za usajili S1133 ni shule ya bweni kwa wavualana na wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, ipo Kata ya Msangani, Kibaha, Kwa Mathias mkoa wa Pwani umbali wa kilomita sita kutoka Barabara Kuu ya Morogoro.

 

Sekondari ya Msangani inapokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kwa michepuo ya HGE, EGM, HGL, ECA na HGK.

 

Shule ipo kwenye mazingira mazuri na tulivu na rafiki kitaaluma, inazungukwa na uoto wa asili na ina walimu wazuri wenye uzoefu na sifa za kutosha, pia ina vitabu na vifaa vyote vya kufundishia, ina viwanja vizuri vya michezo, huduma nzuri ya chakula, malezi na matibabu.

 

Ada zao ni nafuu sana na mzazi au mlezi analipa kwa awamu (installments). Wahi sasa, fomu zinapatikana shuleni Msangani, Riki Hotel – Mnazi Mmoja Dares Salaam, Msimbazi Centre, Palace Hotel Aruisha na Mwanza Soko Kuu duka namba 27 ndani.

Kwa mawasiliano, piga simu namba 0754 655 725 au 0715 655 725.


Loading...

Toa comment