NAI AFUNGUKIA ISHU YA KUJICHUBUA

Nai Kisa ‘Nai’

BAADA ya kuandamwa mitandaoni juu ya ngozi yake kwamba anajichubua, muuza nyago maarufu Bongo, Nai Kisa ‘Nai’ amefungukia ishu hiyo kwamba siyo kweli bali ni kung’aa kwa ngozi yake tu.  

 

Nai ambaye ameuza sura kwenye video kibao Bongo ikiwemo ya Muziki ya Darassa alisema kuwa, watu wengi wamekuwa wakimsema kuwa anauza losheni za kujichubua na ndizo zinazomfanya wakati mwingine kubadilika ngozi yake.

 

“Jamani eeh mimi sijichubui na wala losheni ninazouza sio mkorogo, hii ni kwa ajili ya kung’arisha ngozi yaani uliyonayo inabaki hivyohivyo ila inazidi kung’aa kwa hiyo huwezi kuita mkorogo. Mtu anayetumia mkorogo utamjua tu lazima atakuwa na sugu baadhi ya sehemu sasa mimi sina nina rangi moja mwili mzima utasemaje najichubua tena wanikome,”alisema Nai.

Toa comment