The House of Favourite Newspapers

Naibu Katibu Mkuu Zuhura Awasili Ofisini Rasmi Mtumba jijini Dodoma

0

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus amewasili rasmi ofisini na ameomba kupatiwa ushirikiano na uongozi pamoja na watumishi wa ofisi hiyo ili kumwezesha kutekeleza vyema majukumu yake.

“Ninafuraha kuwepo hapa ninachoomba kutoka kwenu ni ushirikiano wenu,” amesema

Amesema hayo leo Juni 13, 2024 alipowasili katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma, alipokelewa na Katibu Mkuu, Mhe. Mary Maganga, Menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo.

Naye, Katibu Mkuu Maganga ameahidi kumpatia ushirikiano mzuri Naibu Katibu Mkuu Yunus na kuishukuru Menejimenti na watumishi kwa kumpatia mapokezi mazuri na kuwataka wampatie ushirikiano mzuri Naibu Katibu Mkuu huyo ili kumwezesha kutekeleza majukumu yake vyema.

 

 

Leave A Reply