Naibu Waziri Aanika Mazito Wabongo Kuteswa, Kuuawa Uarabuni – Video

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro amesema kuwa baadhi  ya Watazania wanaokwenda nchi za Uarabuni kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali hasa akina dada, wamekua wakipata manyanyaso na wakati mwingine kuuawa kinyama kwa sababu wanatoroka hapa nchini kinyemela na hata wakifika huko hawatoi taarifa kweny balozi husika.

 

Dkt. Ndumbaro ambaye ni mbunge wa Songea Mjini (CCM) amesema hayo leo Ijumaa, Juni 8, 2019 wakati akifanya mazungumzo maalum na kituo cha +255 Global Radio alipotembelea ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

 

“Tumekuwa tukiwaambia watu wote wanaokwenda kufanya kazi Uarabuni waripoti kwa mabazoli wetu kwanza, maana kuna mengi mabaya wanaweza kufanyiwa huko ugenini. Sasa unyama huu unatokea kwa sababu hawafuati taratibu, unakwenda kwenye nchi ya watu wala hujulikani umetoka wapi.

 

“Lakini hatuwaachi, mtu akishaathiriwa na unyanyasaji tunamchukua tunamrudisha nyumbani kibinadamu wala hatumuadhibu. Tangu tumeingia madarakani hili limepungua sana, kuna wengine wanajiita diaspora wamejilipua sana kenda nje, waliondoka kama wakimbizi wa Somalia na kule hawajuliani, wanamuweka balozi kwenye wakati mgumu sana.

 

“Juzi hapa alifariki Mtanzania kule Ubelgiji, hata passport hana, amekaa kule miaka mingi lakini kule wanamfaham,u kama Mnyarwanda, ilibidi ndugu zake watoke Tanzania kenda kutoa maelezo,” amesema Ndumbaro.

  

MSIKIE DKT. NDUMBARO AKIFUNGUKA HAPA

Loading...

Toa comment