The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Apagawisha Siku ya Msanii Kijiji cha Makumbusho

anastanzia-wambura-2-001Naibu Waziri wa wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Anastazia Wambura (kushoto) akicheza muziki wa ‘Segere’,  kulia ni Katibu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mungereza  akimuunga mkono.Viongozi wakiserebuka katika tamasha hilo.anastanzia-wambura-4-001Viongozi wakiserebuka katika tamasha hilo. anastanzia-wambura-3-001Baadhi ya wananchi waliofika katika tamasha hilo wakimuunga mkono Wambura  kwa kucheza.anastanzia-wambura-6-002Wambura akisoma hotuba yake.anastanzia-wambura-7-002…Akisisitiza jambo kwenye hotuba hiyo.anastanzia-wambura-8-002Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba,  akipita mbele ya Wambura kupokea cheti cha mchango wake katika kuongoza.anastanzia-wambura-1-002Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja.anastanzia-wambura-5-002Baadhi ya wananchi waliofika kwenye tamasha hilo.

NAIBU Waziri wa wa Habari,  Utamaduni,  Wasanii na  Michezo, Anastazia Wambura,  jana aliwapagawisha wananchi mbalimbali waliojitokeza katika tamasha la sanaa  alipocheza muziki na kuungwa mkona na mashabiki wengine katika wimbo wa ‘Segere’.

Tukio hilo lilijiri jana jioni katika tamasha la sanaa Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar ambapo pia kulitawaliwa shangwe   na vivutio mbalimbali kama ngoma, mziki wa asili, Bongo Fleva, muziki wa bendi, matarumbeta, sarakasi, vichekesho,  maigizo ya jukwaani na maonyesho ya sanaa za ufundi.

Vivutio vingine ambavyo vilionekana kuvutia ni pamoja na picha za kuchora za mafuta na maji, sanamu za kuchongwa, sanamu za kuungwa kwa vyuma chakavu, vyungu, mikeka, wasusi, ramani na ubunifu wa majengo.

Tamasha hilo la sanaa limefanyika kabla ya maadhimisho ya Siku ya Msanii linalotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, likiwa na lengo la kuwaweka pamoja wasanii wa fanii mbalimbali ili kupata fursa ya kuonyesha kwa wananchi na kujenga uelewa juu ya kazi zao mbalimbali za sanaa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Wambura alisema  anatoa wito kwa wasanii wote  nchini kusajili kazi zao ili kupambana na maharamia wa kazi zao na pia akatumia fursa hiyo kuwaomba waandaaji na BASATA kuhakikisha Siku ya Msanii inaadhimishwa nchi nzima.

Aidha alisema kwa kuwa kuna changamoto ambazo amezisikia kupitia hotuba ya wasanii ikiwemo ukosefu wa sehemu ya kufanyia kazi za sanaa, serikali ya awamu ya tano ipo sambamba na wasanii kuhakikisha wananufaika na kazi zao.

Kuhusu ukosefu wa mitaji alisema  serikali itahakikisha inalifanyia kazi jambo hilo likiwemo linalohusu tozo mbalimbali zisizo za lazima.

Naye Katibu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza,  aliwapongeza waandaaji Haak Neel Production kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wasanii wanakutana na kueleza changamoto zao wanazokabiliwa nazo kwa serikali na kuzifanyia kazi.

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Comments are closed.