The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko Atoa Maagizo Matatu Kuhusu Kazi za Wasanii

0

 NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko ameangiza mambo matatu muhimu kwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro juu ya kazi za wasanii kupata heshima yao.

Hayo aliyazungumza jana katika halfa ya mkutano wa wadau wa mfuko wa Utamaduni na Sanaa uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Johari Rotana kimuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ambaye alitakuwa kuwa mgeni rasmi.

Biteko alisema Wizara inatakiwa kuwaona Wasanii kama nyenzo muhimu katika Taifa kwa sababu Sanaa ni kuelimisha, kuburudisha na sasa imekuwa ni ajira kwa vijana wa Tanzania.

Alisema kushuhurika na wasanii, kazi ya waziri kuwa daraja la kuungani wasanii katika kupata kazi ikiwemo katika makampeni na kulipwa kwa kazi zao na sio Asante.

“Waziri nahitaji kuona katika kazi za Serikali Wasanii wanapewa kazi na kulipwa kwa sababu Sanaa ni ajira na sio kupewa Asante, mabank kurahisisha masharti ya mikopo,” alisema Biteko.

Aliongeza kuwa ukitaka kuliua taifa usihangaike na technology, hangaika na utamaduni wake, ikiwemo lugha yake, chakula chake na hata utamadu wao wa ndoa.

“Wasanii wana kazi kubwa sana ya kulifanya taifa hili kuwa hai kwa kuenzi utamaduni za nchini yetu, kusisitiza juu ya utamaduni yetu. Licha ya kuwepo kwa mambo yetu ndani, basi tusikubali kudhalilisha utamaduni wetu kwa mgeni ambaye anakuja kututembelea,” alisema Naibu Waziri Mkuu.

Alieleza kuwa kazi ya Sanaa ni kuelimisha na kuburudisha hali hiyo wasanii wanatakiwa kutengeneza ajira, hali hiyo Rais Samia kufufua mfuko ambao ulikuwa 1992.

Sekta ya utamaduni inayoongoza kwa ukuwaji kuliko sekta zote nchini imekuwa kwa asilimi 19 lakini imekuwa duni katika mchango wa taifa,” alisema Biteko.

Alisema Wasanii wanaaminika na waendelee kuipa hadhi ya nchini hii, anachukia ujanja ujanja au uongo kuita usanii. Msanii ni uumbaji, Sanaa na usanii ni jambo la heshima.

Wakati huo huo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Damas Ndumbaro alisema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan wanatarajia kutengeneza mji wa Sanaa ambao utakuwa nje ya mji.

Alisema Rais Samia katika kujali na kuwapambania sana alipata nafasi ya kuzungumza na Muigizaji na DJ, Idris Eiba wa Uingereza kwa ajili ya kuja nchini ili kuja kuwekeza.

“Hivi karibuni Rais alipokwenda Uingereza alikutana na Muigizaji huyo hakuna mtu aliyemtua bali ni mapenzi yake na kutaka kuona Sanaa na Utamaduni wetu unakuwa pamoja na wasanii wetu kukuwa zaidi,” alisema Ndumbaro.

Kuhusu mikopo kwa wasanii, alisema 2022 alitoa fedha za mikopo , walikuwa wanakopeshwa katika ofisi ya mfuko, asilimia 70 ya fedha hazijarudishwa katika mfuko kwa sababu haukuwa na dhamana.

“Rais kwa nia njema alitoa maelekezo kuwa mikopo yanatolewa Bank na wanadai na dhamana, wasanii ndio walisababisha mikopo kwenda huko na kufuata utaratibu sahihi,” alisema Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.

Aliongeza kuwa wako katika mchakato wa kutunisha zaidi mfuko wa kodi zote wanazolipa wasanii na kutoa asilimia ndogo kwa ajili ya kutanua mfuko huo ili kuweza kuwakopesha zaidi.

Leave A Reply