Naibu Waziri Ndumbaro Kuhusu Ushoga: “Sio Makonda tu, Hata Trump” – Video

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro akifanya mahojiano na kituo cha +255 Global Radio alipotembelea ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar leo.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro amesema kuwa baadhi  ya Watazania wamekuwa wakichukua mambo juujuu na kuyashadadia mitandaoni bila kufanya uchunguzi wala kufuatilia kwa kina huku akitolea mfano suala la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kuwataka waliotajwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga) kuripoti kituo cha polisi.

 

Dkt. Ndumbaro ambaye ni mbunge wa Songea Mjini (CCM) amesema hayo leo Ijumaa, Juni 8, 2019 wakati akifanya mazungumzo maalum na kituo cha +255 Global Radio alipotembelea ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Meneja wa kituo cha +255 Global Radio, Borry Mbaraka,  akifanya mahojiano na Dkt Ndumbaro.

“Kauli ya kudhibiti ushoga iliyotolewa na Makonda iliibua taharuki na kuwasha moto nchi nzima, lakini watu wamesahau kwamba hata Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akisema kauli kama hiyo ya kudhibiti mashoga mara nyingi tu lakini haizungumziwi sana hapa kwetu.

 

“Tusikubali kununuliwa kuichafua nchi yetu, ni mambo mengi yanapangwa ili kuichafua Tanzania sababu watu wameshindwa kuchukua raslimali zetu. Lakini niwahakikishie kwamba taswira ya Tanzania kwa nchi za nje ni kubwa sana,  imejengwa tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally akiwa katika picha na Dkt  Ndumbaro.

Kuhusu fani yake ya sheria kwa vile sasa ni waziri, alisema:

“Sijaachana na masuala ya sheria wala michezo, bali kea sasa ninafanya sheria na michezo kimataifa zaidi. Sote tunafahamu kwamba, wanasiasa ndiyo wanaongoza nchi, na miaka ya nyuma wengi waliamini kwamba siasa ni ujanjaujanja lakini siyo hivyo, Rais Dkt. John Magufuli ndiye amenishawishi kuingia kwenye siasa kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye hili taifa.

 

“Baadhi ya wawekezaji kutoka nje hawapendi taifa letu liendelee, wanaona wivu kutokana na raslimali nyingi zilizomo kwenye taifa hili, kwa hiyo wanatumia mbinu za rushwa kuwahonga wanaofanya maamuzi ili wawekeze kwenye maeneo mbalimbali zikiwemo fukwe, madini, utalii, bandari na maeneo mengine.

 

MSIKIE DKT. NDUMBARO AKIFUNGUKA HAPA

Loading...

Toa comment