Naj: Siwezi kurudi kwa Mr Blue wala Diamond
Stori: HAMIDA HASSAN
UKWELI kabisa! Msanii anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Najma Dattan ‘Naj’ aliyewahi kuwa na uhusiano na Herry Samir ‘Mr Blue’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kwa sasa hana mpango na wanaume wa Bongo tena kwa sababu amegundua kuwa si wa kweli.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Naj alisema kuwa baada ya kujaribu kuingia kwenye uhusiano na wanaume wa Bongo aligundua ni waongo hivyo alipata funzo.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Kuna watu wanadhani nimerudi kuharibu uhusiano wao, mimi kwa Mr Blue na kwa Diamond siwezi kurudi, naheshimu uhusiano walionao kwa sasa.



