The House of Favourite Newspapers

Najma: Nikiwa faragha na mpenzi, napenda kulala kifuani

0

Unamkumba vizuri mwanadada Najma aliyewahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mr. Blue na Diamond Platnumz? Jina lake kamili anaitwa Najma Dattan.

Kwa sasa mwanadada huyu anafanya muziki na hivi karibuni Mwandishi Wetu Hamida Hassan alimnasa na kumpiga maswali 10, bila hiyana aliyajibu kwa ufasaha.

Ijumaa: Najma leo ndiyo mara ya kwanza unaingia kwenye safu hii, naomba uwaeleze wasomaji ni kweli umewahi kuingia kwenye uhusiano na Mr Blue, na kama ni kweli, kwa nini mliachana?

Najma: Hakuna la kuficha alikuwa mpenzi wangu nikiwa na umri wa miaka 15, tuliachana kitambo lakini sipendi kumuongelea zaidi.

Ijumaa: Vipi kuhusiana na mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mliwahi kuwa wapenzi?

Najma: Sijawahi kuwa na uhusiano na Diamond, alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana na muda mwingi nilikuwa naye studio ndiyo sababu ya watu kusema nina uhusiano naye.

Ijumaa: Mbona waandishi waliwahi kukufumania kwa dada yako ‘Lady Na’, lakini hamkuwahi kulizungumzia, ukweli ni upi?

Najma: Nimesema Diamond alikuwa mtu wangu wa karibu, sina zaidi.

Ijumaa: Mara nyingi huonekani, unaishi nje ya nchi?

Najma: Yeah, naishi London, kikazi lakini kwa sasa nipo hapa kukamilisha albamu yangu, kwa sasa hapa ni kazi tu.

Ijumaa: Umejipangaje kupambana na ushindani uliopo kwenye muziki?

Najma: Niko ‘fiti’ japo sipo kwa ajili ya kushindana na mtu, kazi yangu mpya nimefanya na Chameleon, muda si mrefu itakuwa hewani.

Ijumaa: Unaweza kuwakumbusha wasomaji wimbo wako wa kwanza na kama kuna ambao umetoa hivi karibuni?

Najma:  Wa kwanza unaitwa Don’t Let Me Go, wa sasa unaitwa No Going Home, ambao niliurekodia kwa Said Fella lakini video yake nimeifanyia jijini London.

Ijumaa: Vipi, una mpenzi?

Najma: (Huku akiachia tabasamu), no, sina na wala sihitaji.

Ijumaa: Ni mwanaume mwenye vigezo gani unayemhitaji maishani mwako?

Najma: Mwanaume mwenye heshima, upendo wa dhati, mchapa kazi, mwenye elimu na zaidi ya yote awe na hofu ya Mungu.

Ijumaa: Ungependa kuzaa watoto wangapi?

Najma: (Kicheko), watano, lakini hata nikijaaliwa watatu, nitashukuru.

Ijumaa: Ukiwa faragha na mpenzi wako unapenda kukaa naye kwa pozi gani na huwa unavaa nguo ya aina gani?

Najma: Napenda kulala kifuani kwake na vazi nilipendalo katika mazingira hayo ni tisheti tu.

Leave A Reply