The House of Favourite Newspapers

Namungo Fc Yaishushia Mvua ya Mabao De Agosto

0

 

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF)  Afrika Namungo FC  imejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi  baada ya kupata ushindi wa mabao 6-2  dhidi ya wapinzani wao Club Desportivo 1º de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano.

 

Mchezo huo umechezwa leo Feb. 21 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, ambapo Agosto walikuwa wenyeji baada ya CAF kuamua mechi zote zichezwa Tanzania.

 

Wenyeji walipata bao kwa njia ya Penalti dk.11 Moya na la pili limefungwa Dk.50 Salvador huku Mabao ya Namungo FC  yamefungwa na Hashim Manyanya dak.29, Sixtus Sabilo dk.37 na 60 aliyefunga mawili,Reliants Lusajo dk.55,Erick Kwizera dk.65 na Steven Sey dk.70.

 

Kwa ushindi huo Namungo wanasubiri Mchezo wa marudiano utakaochezwa uwanja huo huo wa Chamazi huku wakiwa wenyeji utakaopigwa Februari 25 mwaka huu.

 

Leave A Reply