The House of Favourite Newspapers

Namungo Inajifua Balaa Huko Karatu

0

KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amefurahishwa na maendeleo ya kambi ya timu iyo ambayo wameweka huko Karatu mkoani Arusha wakijiandaa na msimu ujao.


Namungo imeweka kambi
ya siku 14 Karatu katika kituo cha michezo cha Black Rhino kutokana na kuvutiwa na hali ya utulivu uliopo eneo hilo ambapo wanaamini wachezaji watapata wakati mzuri wa kujifua.

Morocco alisema: “Tunamshukuru Mungu wachezaji wote ni wazima na tunaendelea na programu zetu, baada ya siku 14 kuisha tutarudi nyumbani lakini tukiwa tunarudi tutapita njiani kucheza mechi ya
kirafiki.


“Kwa sasa tunaangalia
jinsi ya kujenga muunganiko mzuri wa timu ili kuhakikisha tuna kikosi bora zaidi.

Stori na Lidia Kaaya na Michael Yusuph

Leave A Reply