The House of Favourite Newspapers

Namungo Yaitishia Simba Leo Jumanne Kwenye Dimba la Ilulu, Lindi Ligi Kuu Bara

0

 

KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaochezwa leo Jumanne kwenye Dimba la Ilulu, Lindi, Mtendaji Mkuu wa Namungo, Omary Kaya, amesema watatoa upinzani wa kutosha ndani ya dakika tisini.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaya alisema: “Timu imejianda vema na tunategemea kutoa upinzani wa kutosha tukiingia na malengo ya kutafuta pointi tatu.”

 

Kwa upande wa mshambuliaji wa Namungo, Reliants Lusajo, alisema: “Kikubwa kwa upande wetu sisi wachezaji tumejiandaa vizuri, tunawaheshimu wapinzani wetu kwa sababu ni timu kubwa, hivyo lazima tucheze kwa kuwaheshimu, naamini tutaenda kupambana kwa ajili ya kupata pointi tatu.”

 

Namungo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikifanikiwa kukusanya pointi 29 kwenye michezo 21, huku Simba wakiwa wa pili na pointi 42. Wamecheza mechi 20.

STORI NA NAILA SHOMARI

Leave A Reply