Namungo Yampigia Hesabu Salamba

IMEBAINIKA kuwa nyota wa Simba, Adam Salamba amekuwa akiwindwa na klabu ya Namungo FC ambayo imepanda daraja pamoja na timu ambayo amewahi kuichezea na Lipuli FC.

 

Salamba amekuwa akitajwa kuwa ni mchezaji wa simba ambaye Kocha Patrick Aussems hana mpango naye kwa msimu ujao wa ligi na huenda akachwaa au kutolewa kwa mkopo.

 

Hivyo amekuwa akiwindwa na klabu ya Namungo ambayo ndiyo kwanza imepanda daraja ambayo imeanza mipango yake ya usajili.

 

Taarifa zinadai kuwa nyota huyo huenda akawa Namungo hata kwa mkopo kama wataafikiana na simba kwa ajili ya msimu ujao. Spoti Xtra ilizungumza na mchezaji huyo wa simba, Adam salamba ambaye alifunguka: “Mimi ni mchezaji wa simba hayo unayoyasema sifahamu na sasa bado ni mapema sana mambo ya usajili.”

Toa comment