Namungo Yasajili Straika wa Vital’O

UONGOZI wa Namungo FC, juzi usiku ulikamilisha usajili wa mshambuliaji wa Vital’O ya Burundi, Jerome Sina na kiungo wa Bugesera ya Rwanda, Steve Nzigamasabo kwa mkataba wa miaka miwili kila mmoja.

 

Mbali ya nyota hao, timu hiyo imefanikiwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo wake, John Mbise kufuatia mchango mkubwa alioutoa katika Ligi Daraja la Kwanza kabla ya kupanda ligi kuu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha wa timu hiyo, Hitimana Thierry raia wa Rwanda alisema kuwa wamesajili nyota hao kutoka katika mataifa hayo kwa lengo la kukiongezea nguvu kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

 

“Tayari nipo zangu huku Ruangwa kwa ajili ya kuanza maandalizi lakini nimekuja na wachezaji wawili wa kigeni ambao wameshasaini mkataba wa miaka miwili, yupo anayetoka Burundi na anayetoka Rwanda.

 

“Unajua lengo ni kuwa na timu imara ambayo italeta ushindani ndiyo maana tumewaongeza na hao, huyu anayetoka Rwanda ana uwezo wa kucheza kama kiungo na anayetoka Burundi anauwezo wa kucheza katika nafasi zote za ushambuliaji,” alisema Thierry

Loading...

Toa comment