The House of Favourite Newspapers

Nanah Uzuri Wangu Unanitesa

0

VIDEO queen maarufu Bongo Nabila Othman ‘Nanah’ amesema urembo alionao unamtesa kwa sababu kuna muda anafuatwa na wanawake wenzie na kuambiwa anatembea na waume zao jambo ambalo sio kweli.

 

Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili Nanah aliyewahi kufanya vizuri kwenye wimbo wa I love you wa Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ aliendelea kueleza kwamba kuna muda anaweza akawa amekaa na mwanaume wanajadili mambo ya kazi lakini kutokana na uzuri alionao mwanamke wake anaanza kuhisi anatoka na mwanaume wake.“

Kuna muda huu uzuri unanitesa,ndio kama hivyo naweza nikakutana na mwaname kwa ajili yakujadili mambo ya kazi lakini watu wakafikiria tofauti, huwa inanikera sana kwa sababu binafsi najiheshimu na siwezi kutoka na kila mwanaume ikiwa sijampenda, kwa hiyo naomba watu wasinichukulie tofauti hasa wale ambao wanaona nipo na waume zao, jamani ni kwa ajili ya kazi tu na sio vinginevyo,” alisema Nanah

Leave A Reply