The House of Favourite Newspapers

Nandy Afunguka Kuhusu Rayvanny Kulipishwa Milioni 50 WCB

0
Rayvanny akiwa katika Jukwaa la Nandy Festival mjini Songea

MSANII wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘nandy’ ameeleza kusikitishwa kwake baada ya kupata taarifa kuwa msanii mwenzake Rayvanny ametakiwa kulipa pesa kiasi cha Tsh milioni 50 kwa sababu alikwenda kufanya shoo kwenye Nandy Festival mjini Songea ilihali hajamalizana kikamilifu na lebo yake ya awali ya Wasafi.

 

Nandy amesema taarifa hizo zilimuumiza na kuhisi yeye ndiye amemsababishia matatizo kwani alimtafuta yeye na kumuomba aende akampe kampani kwenye tamasha lake hilo.

 

“Rayvanny na mume wangu ni marafiki sana, mume wangu anakwenda sana Next Level Studio wanafanya kazi zao, na mimi na mama mtoto wake Fahyma ni rafiki yangu sana, tuna ule ufamilia. Kwa hiyo nilikuwa nimempeleka mume wangu pale Next Level, nikamtania tu kwa nini Ray usije kwenye Nandy Festival? Akasema tutaongea.

Taarifa zinadai Rayvanny anatakiwa kulipa kiasi cha Shilingi Milioni 50 kwa WCB

“Baadaye Billnass akaniambia kitu ulichoongea na Rayvanny nadhani kina make sense, lakini ukifanya kama sapraizi itapendeza zaidi. Nilipompigia kumwambia akasema ana shoo ‘lakini kwa sababu ni marafiki, nitakuja na timu yangu’.

 

“Hii ni biashara, kwa hiyo tulifuata masharti ya vigezo vya management, alikuja na timu yake ya watu 13, kwa hiyo nikaelewa kweli hii ni biashara na alilipwa pesa, Hatukuwahi kuongelea masuala ya WCB niliongea naye yeye kama yeye.

Nandy

“Kuhusu taarifa za kwamba anatakiwa alipe WCB kwa sababu alikuja kwenye shoo yangu kiukweli nimejisikia vibaya, naona kama nimemsababishia, nimeshindwa hata kumuuliza.

 

“Lakini niliona kwenye mitandao ameandika kwamba ni msanii huru kwa hiyo nikapata relief kwamba yawezekana yaliyokuwa yanazungumzwa ni mambo ya mitandaoni tu,” amesema Nandy.

Leave A Reply