The House of Favourite Newspapers

Nandy Alamba Ubalozi Sabuni Mpya za Azania Group

 

 

 

Nandy akibadilishana mikataba na uongozi wa Azania Group..

MAKAMPUNI ya Azania Group yanayomiliki Kampuni kubwa ya bidhaa za chakula nchini, leo Oktoba 10, 2019 imezindua sabuni zake mpya za unga ya King Limau na King Marhaba zenye ubora wa kimataifa na kumsainisha mkataba wa kuwa balozi wa bidhaa hiyo mwanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles maafuru kama ‘Nandy’.

Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea.

Tukio la kutiliana saini za mkataba wa kuitangaza bidhaa hiyo limefanyika Hoteli ya Hytt Regency, Kilimanjaro Hotel, ambapo Meneja uendelezaji wa kampuni hiyo, Joel Laiser amesema sabuni hizo ni bor, zenye ubunifu na kuondoa kila aina ya uchafu pale zinapotumika.

 

Laiser amewashauri Watanzania kutumia King Limau na King Marhaba kwa sababu licha ya ubora wake unaojidhihirisha, bado sabuni hizo zinbauzwa kwa bei chee.

 

Nandy akitiliana saini na uongozi wa kampuni hiyo.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Nandy alisema kabla ya kuingia mkataba wa kuwa balozi wa sabuni hizo, alianza kuitumia King Limau na King Marhaba kwa zaidi ya wiki tatu na kujidhihirishia ubora wake ndipo akaukubali ubalozi huo.

 

Nandy akionesha sabuni hizo baada ya kuingia mkataba.

Nandy alieleza kuwa unapotumia sabuni hizo kufulia hazichubui mikono wala kufubaza nguo kama zingine pia zina harufu nzuri.

Nandy akielezea ubora wa sabuni hiyo baada ya kuitumia kwa wiki tatu kabla kuingia mkataba huo.

“Katika matumizi ya sabuni siku zote mimi huwa napendaga sana yenye harufu nzuri, na hilo ndiyo jambo lililonifurahisha kwenye sabuni hizi,” alisma Nandy.

Sehemu ya sabuni hizo.

Laizer akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.

Meneja uendelezaji wa Makampuni ya Azania Group, Joel Laizer akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Nandy akigawa sabuni hizo kwa wageni waalikwa nao wakajionee ubora wake.

Nandy akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa kampuni hiyo.

HABARI/PICHA: NEEMA ADRIAN /GPL 

 

Comments are closed.