The House of Favourite Newspapers

Nandy Aliapa Kutafuta Pesa kwa Ajili ya Kumheshimisha Billnass-Abdulrazack

0
Mshauri wa masuala ya mahusiano Sheikh Abdulrazack

MSHAURI wa masuala ya mahusiano Sheikh Abdulrazack amefichua siri ambayo ilikuwa haifahamiki miongoni mwa mashabiki wengi wa muziki nchini kuhusu namna wasanii wawili Billnass pamoja na Nandy safari yao ya uhusiano ilivyoanza hadi hapo ilipofikia.

 

Sheikh Abdulrazack amesema kuwa wakati Nandy akiwa na Billnass alihisi watu wengi walikuwa wakimdharau mume wake wa sasa ambaye kwa kipindihicho alikuwa ni mpenzi wake ndipo alipojiapisha kutafuta pesa kwa namna yoyote ile awezayo ili aweze kuhakikisha anamsaidia Billnass kukuza uchumi wake binafsi ili aheshimike.

 

Sheikh Abdulrazack akiwa ndani ya Studio za Global TV na Global Radio

“Kuna kauli aliwahi kuisema kuwa watu wanamdharau Billnass lakini ntatafuta hela kwa sababu yake na huyu ndiye atakayenioa, kwahiyo alifanya kila kitu kwenye maisha yake kuhakikisha kuwa Billnass naye anainuka naye.” amesema Sheikh Abdulrazack.

Billnass na Nandy kwa sasa ni Mume na Mke

Mtaalamu huyu ameendelea kwa kusisitiza kuwa kutokana na adhima aliyokuwa nayo Nandy amejitahidi hadi kufanikiwa kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kumuweka Billnass hapo alipo pamoja na kutimiza ndoto yake ya kuwa mke wa Billnass.

Leave A Reply