The House of Favourite Newspapers

Nandy aonesha jeuri ya fedha

0

MWENYE nacho ataongezewa! Ndivyo msanii Bongo wa Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ (26), anavyozidi kuonesha jeuri ya fedha.  Usikumbuke mjengo wa kisasa na magari ya kifahari aliyowahi kuripotiwa kumiliki, hivi sasa chanzo kinasema mrembo huyo anazidi kunukia fedha. Ilikuwa kama tipu tu ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita Nandy alitupia picha ya gari jipya aina ya Toyota IST kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo wapambe wake walianza kumpongeza kwa kununua gari hilo.

Kama hiyo haitoshi kwenye mitandao mingine ya kijamii mashabiki wa mrembo huyo walitupia picha iliyomuonesha akiwa ameweka meno ya bandia. Baadaye ishu ikavuja kutoka kwa vyanzo vya habari kuwa msanii huyo amenunua meno hayo kwa gharama ya shillingi milioni 63.

Ishu hiyo ilipomfikia mwandishi wetu aliwasiliana na Nandy kwa njia ya meseji akimpongeza kwa mafanikio makubwa sambamba na kununua gari hiyo ambapo alijibu: “Hahahah, asante jamani,” na kuacha kufafanua zaidi. Hata hivyo rafiki yake wa karibu alimwambia mwandishi wetu kuwa kwa sasa mrembo huyo hakamatiki kwa mkwanja na maisha ya bata. “Nandy si mtu wa kawaida kwa sasa, binafsi kama rafiki nakiri kwamba fedha imemtembelea.”

Hivi karibuni msanii huyo aliwahi kumuonesha mwandishi wetu gari la kifahari aina ya Land Rover Discover TDV6 HSE sambamba na kadi iliyoonesha kuwa ndiye mmiliki.

Chanzo kinaeleza kuwa, siku chache zilizopita msanii huyo baada ya kuweka meno ya madini ya almasi yenye thamani ya millioni 63 za Kitanzania na gari dogo aina ya IST kwa ajili ya kutembelea alienda nchini Kenya kwa ajili ya mapumziko.

“Ni kweli amenunua hilo gari anasema si kila mahali mtu unaweza kwenda na gari la kifahari, sehemu nyingine unatakiwa kwenda ‘simpo’ na IST ndiyo aliyoichagua,” chanzo kilisema.

Mbali na magari hayo mawili mrembo huyo anayesumbua na Wimbo wa Nigande, katika orodha yake hiyo ya magari, limo BMW X1, Mercedes Benz E-Class E320 CDI, Toyota Alphard, Toyota Harrier na Toyota Noah ambayo yote huwa anayatumia kwa shughuli zake mbalimbali.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni mrembo huyo ameweka wazi siri ya mafanikio yake kuwa ni kujituma na kujiwekea malengo katika kazi zake. “Siri ya mafanikio yangu inatokana na juhudi zangu. Pia nina menejimenti nzuri ambayo ipo siriazi sana linapokuja suala la kazi, ndiyo maana imenifanya niwe na mafanikio haya,” alisema Nandy.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko linafahamu kuwa msanii huyo ana kampuni ya bidhaa za urembo na pia ni balozi wa kinywaji kikubwa Afrika Mashariki. Aidha katika siku za hivi karibuni Nandy amezidi kukua kimuziki kiasi cha kufikia kupiga shoo katika viwanja vya mpira kama alivyofanya mkoani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani

STORI :Memorise Richard, Risasi

Leave A Reply