Kartra

Nandy Aonyesha Pete ya Uchumba

Malkia wa muziki wa Bongo Fleva kwa sasa Afrika Mashariki na Kati, Nandy ameamua kwenda kula bata  la hatari huko Dubai au Dubenga Falme za Kiarabu kwenye maraha ya dunia.

Hata hivyo, ubuyu mpya mjini ni kwamba yupo kipande hicho na mchumba’ke, Billnass au Nenga. Kinachoaminisha wengi kuhusu ubuyu huo ni baada ya lokesheni na picha za walipo kufanana huku Nandy akionekana zaidi kwenye kula bata sehemu za jangwani, hotelini na kwenye matamasha ya asili ya Kiarabu.

Wawili hao wamekuwa wakidaiwa kumwagana kisha kurudiana tangu walipovishana pete ya uchumba mwaka juzi kabla ya baadaye Nandy kudai kuipoteza pete hiyo.

Unaambiwa safari ya Dubai inaweza kuwa imezaa matunda kwa couple ya Nandy na Billnass baada ya kuonyesha pete nyingine ya uchumba baada ya ile ya zamani kupotea. Kupitia Insta story ya The African Princess, Nandy ame-share sehemu ya video akionesha pete hiyo kwa mashabiki.

Cc; @sifaelpaul

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)


Toa comment