NANDY ATOBOA SIRI YAKE NA MOBETO

Faustina Charles ‘Nandy’

HITMAKER wa Ngoma ya Ninogeshe, Faustina Charles ‘Nandy’ ametoboa siri yake na mwanamitindo Bongo, Hamisa Mobeto kuwa wapo mbioni kufanya ziara ya pamoja nchini Marekani wakiongozana na Aslay.

Akifanyiwa mahojiano na Ijumaa, Nandy alisema; “Natarajia kusafiri siku ya tarehe 25 mwezi huu kuelekea Marekani kwa ajili yakufanya ziara nikiwa na msanii mwenzangu Aslay na Hamisa kisha nitarudi Bongo tarehe 10, Desemba tukiwa wote watatu, pia hii kwangu itakuwa ni mara ya kwanza kufika huko kwa sababu sijawahi kwenda kabisa,”alisema Nandy.

Stori: Memorise Richard

Toa comment