The House of Favourite Newspapers

Nandy Awaomba Watanzania Msamaha Kwa Walichokiona

Mwanamuziki Faustina Charles ‘Nandy’  na mwanamuziki mwenzake, Billnas.

BAADA ya kuvuja kwa video inayowaonyesha wanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’  na Billnas wakiwa faragha na  ambayo imezua gumzo leo katika mitandao ya kijamii, Nandy   amekiri kwamba video hiyo ni ya kweli japo ni ya mwaka 2016 na amewaomba  msamaha Watanzania kwa walioiona video hiyo.

 

Akifunguka  zaidi, amesema video hiyo ilichukuliwa akiwa katika uhusiano na Billnas ambapo walikubaliana iwe ya siri.

 

“Sielewi ana maana gani kuitoa video hiyo kwa sasa na kufika kwenye mitandao, kwani vitu kama hivi vinafanyika kwa mtu yeyote anayekuwa kwenye mahusiano,” amesema.

Wakifanya yao.

“Nimesikitishwa sana na kitendo hicho na ‘ilishutiwa’ kwa mtindo wa ‘Snapchat’ na sijui kwa nini ameamua kuirusha sasa hivi, yaani sielewi nifanye nini.  Nawaomba radhi kwa mashabiki wangu, familia yangu, kanisani kwangu na serikali.  Kiukweli video imenichafua sana ila adhabu ya maumivu haya ninayoyapata sasa hivi ni kutokana na kumuamini Billnas.

Comments are closed.