Nandy: Billnass Punguza Mapenzi Utaniua! Ndoa Mpya Ndiyo Tamu Hivi

SUPASTAA wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘nandy’ ameamua kufunguka ya moyoni kuhusu mahaba anayopewa na mumewe ambaye pia ni msanii mwenzake, William Lyimo ‘Billnass’ katika maisha yao ya ndoa waliyoyaanza hivi karibuni.

 

Nandy ambaye ni mama kijacho ame kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza ni kiasi gani kwa sasa anaenjoy kwenye ndoa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mumewe huyo huku akimtaka apunguze kidogo.

Nandy na Billnass

Nandy ameandika; ”Nyie ndoa ikiwa mpya ndo mapenzi yanazidi hivi??? Jamaaaani nimetepetaaaaaa @billnass jamaaan mume wangu punguza mapenzi jamani utaniua.”

 

Ikumbukwe kuwa, mastaa hao wana takribani mwezi mmoja tangu wafunge ndoa yao Julai 16, 2022 na sasa wanatarajia kupata mtoto wa kwanza.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment