Nandy, Lulu Diva Wamuumbua Gigy Money!

BAADA ya kuwepo kwa tetesi za bifu zito kati ya wanamuziki wawili wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, mbivu na mbichi zimejulikana huku mwenzao, Gift Stanford ‘Gigy Money’ akiumbuka.

 

Hivi karibuni, Gigy alisikika akisema kuwa, Nandy alimuibia Lulu Diva dili fulani na ndiyo sababu wakawa kwenye bifu zito.

 

Hata hivyo, katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Lulu Diva alikanusha kwamba, hajawahi kuwa na wala hana ugomvi na Nandy. Lulu Diva amesema yeye na Nandy hawana tatizo na wako sawa, ila ni maneno tu yanatengenezwa na watu.

 

“Mimi na Nandy hatujawahi kugombana, maneno yapo, unaletewa hili, unaletewa lile. Kama watoto wa kike, unalichukua unaliweka moyoni na mkikutana, unamuona mwenzako mbaya.

 

“Sina roho ya kinyongo. Ni mtu wa kusapoti kwenye jambo zuri na ndiyo sababu ya kunialika kwenye sherehe ya uzinduzi wa ofi si yake na nimeweza kufi ka,’’ alisema Lulu Diva. Kwa upande wake, Nandy alifunguka kuhusiana na ishu hiyo na kusema kuwa maneno yapo tu.

 

“Maneno kama wasichana yapo tu, ila ni jinsi wewe unavyolichukulia jambo, sisi wote ni watu wazima hadi tunashirikiana na vitu hivyo havina maana kwenye maisha, nashukuru Lulu alivyokuja kunisapoti,’’ alisema Nandy.

 

Mbali na hilo, inasemekana sababu nyingine ni baada ya Lulu Diva kumuiga Nandy kufungua biashara ya kuuza na kusambaza samaki kama afanyavyo Nandy ambaye anajihusisha na kuuza na kusambaza nyama.

Toa comment