The House of Favourite Newspapers

Nandy: Mapenzi Yanatuumiza

0

NANDY The African Princess; ni msanii bora wa muziki Afrika Mashariki ambaye ameamua kuwaweka sawa wale wote wanaodhani yeye anafanya kiki au labda kweli uhusiano wake na Billnass au Nenga umevunjika.

Hii ni baada ya siku za hivi karibuni kuonekana akiposti vitu kama mtu aliyeumizwa katika mapenzi huku yeye akisema anafanya hivyo ili kuwakomboa wale wanaoumizwa na mapenzi, halafu hawana pakusemea. Nandy anasema;

“Mara kiki… Mara pole, mara hivi, mara vile jamani nitaongea, nitasema kinachoniumiza! Msinihukumu kabla sijaongea! Me siyo msanii wa kiki, najiamini mziki wangu.

Ila haya yote ninayoyafanya ni kwa ajili ya Watanzania wote wanaopitia maumivu makali ya mapenzi. “Nimepata DM nyingi, nimepata SMS za kawaida nyingi, simu nyingi…Nyiye watu wana matatizo ya maumivu, wanakufa nayo moyoni tu!! Tusipoongea sisi vioo vya jamii nani ataongea? Lazima tufunguke ili tuokoe vizazi na vizazi.

Haya mapenzi yapo tu kwa nini yanatuumiza hivyo?”

Leave A Reply