The House of Favourite Newspapers

Nandy: Nilikata Tamaa Nikiwa B-Band

0
Fausta Charles ‘Nandy’.

MKALI wa Ngoma ya Wasikudanganye, Fausta Charles ‘Nandy’, kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa, katika maisha yake ya muziki amewahi kukata tamaa ya kutokuendelea na muziki alipokuwa akiimba B-Band.

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Nandy alifunguka kuwa, alikuwa akiamini hawezi kufika mbali kimuziki alipokuwa na bendi hiyo inayomilikiwa na mkali wa Bongo Fleva, Banana Zorro kwa kuwa bado alijiona ana safari ndefu.

“Nilikuwa kwenye hali mbaya kimuziki, nilikata tamaa kwa kiwango kikubwa nikiwa chini ya B Band, lakini tumaini jipya likaibuka moyoni baada ya kuingia kwenye mashindano ya Tecno Own Stage ambapo niliibuka mshindi wa pili na kupata mwanga mpya kimuziki hadi leo,” alisema Nandy.

Mobeto: Diamond Hana Mwanamke Anayempenda Zaidi Yangu!

Leave A Reply