Nandy: Sioni cha Kummisi Billinas

Faustina Charles ‘Nandy’.

MWANADADA anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa, hana kitu alichokisahau au kukikumbuka kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii, Billinas.

 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Nandy alisema kuwa, licha ya kuwa kwenye uhusiano na msanii huyo kwa kipindi kirefu na baadaye kumwagana, haoni kitu chochote cha kukumbuka kwa mwanaume huyo, zaidi ya kuwaza kuongeza juhudi kwenye muziki wake.

 

Billinas.

“Sina ninachoweza kukisahau wala kukikumbuka kwa Billinas, kwa sasa sipo naye karibu kihivyo, namuheshimu kama msanii mwenzangu na si zaidi, muda ukifika nitamuanika mpenzi wangu wa sasa na kuweka wazi jinsi anavyonisapoti kwenye kazi zangu,” alisema Nandy.

 

STORI: MAYASA MARIWATA | RISASI JUMAMOSI

=====

Mke wa R.O.M.A Amlipua Mbunge LIVE, Kisa ‘Zimbabwe’ (VIDEO)


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment