NANDY AVUNJA UKIMYA ISHU YA MIMBA YAKE

BAADA ya habari kuzagaa kuwa ana mimba, mrembo anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amevunja ukimya na kueleza ukweli.

 

Akibonga na Mikito Nusunusu, Nandy alisema kuwa hana mimba bali amekuwa na kitambi tu ambacho kinamkosesha raha kwani watu wengi wanajua kuwa ni mama kijacho.

 

“Jamani sina mimba, hiki kitambi tu sijui hata kimetokea wapi, hivi nafanya mpango wa kukipunguza maana kinanikosesha raha na kila mtu anaamini nina mimba jambo ambalo si kweli kwani sina mpango wa kupata mtoto kabla ya ndoa,” alisema Nandy.


Loading...

Toa comment