Nandy, Zuchu vs Wanigeria Hapatoshi

Hapatoshi! Ndivyo unavyoweza kusema kwenye mpambano wa wasanii wa kike wanaofanya vizuri Bongo, Nandy na Zuchu wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za AEAUSA katika Kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika ambapo wana kibarua cha kupambana na Wanigeria.
Nandy na Zuchu kwenye kipengele hicho wanachuana na wakali wengine kutoka mataifa tofauti lakini zaidi ni Nigeria kama Tiwa Savege, Yemi Alade, Teni, Simi Tems na wengine kutoka nchi nyingine kama Sherine wa Misri na Busiswa wa Afrika Kusini.
Cc; @sifaelpaul

