The House of Favourite Newspapers

Nani amewanyonga watoto hawa wa polisi

0

watoto wanyongwa (7)Marehemu Raphael Sammy.

Na Issa Mnally, UWAZI

DAR ES SALAAM: Ni unyama, ukatili wa aina yake! Malaika hawa wa Mungu walikosea wapi mpaka kuadhibiwa vikali?! Ni watoto wawili wa familia mbili, Julius Dominic (3) na Raphael Sammy (3) ambao mabaki ya miili yao ilikutwa wiki iliyopita kwenye Barabara ya Mwakalinga, Keko, jijini Dar ambapo ripoti ya awali kutoka kwa madaktari ilidai, walinyongwa, Uwazi linakupa zaidi.

Marehemu hao walikuwa wakiishi na wazazi wao ambao wote, yaani baba, mama ni askari wa jeshi la polisi Temeke katika kota zao zilizopo Kambi ya Polisi Ufundi, Kurasini jijini Dar.

watoto wanyongwa (6)Marehemu Julius Dominic.

WALIANZA KWA KUTEKWA

Akizungumza na gazeti hili huku akiombwa kufichwa jina lake kwa vile yeye si msemaji wa familia, mtu mmoja aliyekuwa kwenye maombolezo hayo alisema:

“Kuhusu kutekwa kwa watoto wale hakuna ubishi kwani kwa umri wao, haiwezekani kwamba waliondoka nyumbani peke yao.

watoto wanyongwa (2)Familia ikizika mabaki ya miili ya marehemu

“Lazima kuna mtu au watu waliwateka kwanza, wakaondoka nao kwenye gari maana wangeondoka nao kwa miguu, watu wangewaona na wangesema. Kumfanyia mtoto yeyote asiyejitambua kitendo chochote cha kummiliki na kumdhuru ni kumteka.

“Wale kuna mawili, huenda ni visasi au ni ushirikina. Unajua watoto kutoweka huku Kilwa Road Kurasini halafu wakapatikana kule Keko ni mbali sana! Lazima kuna ishu ndani yake. Sijui ni nani amewanyonga wale watoto?”

BABA MZAZI AZUNGUMZA

Akizungumza kwa masikitiko makubwa na Uwazi nyumbani kwake, baba mzazi wa Julius, Dominic Alphonce alisema kuwa, watoto hao ambao walikuwa marafiki sana walitoweka kambini hapo, Oktoba 26, mwaka jana na walijitahidi kuwatafuta bila mafanikio.

watoto wanyongwa (1)

SIKIA SIMULIZI HII

“Ilikuwa Oktoba 26, mwaka jana, ndiyo siku waliyopotea. Mimi nilikuwa Mbagala ambako nilikuwa nikisimamia uchaguzi mkuu, mke wangu ambaye pia ni askari alikuwa akisimamia Temeke.

“Muda wa saa nane mchana, nikapigiwa simu,  nikaambiwa Juli (Julius) haonekani nyumbani. Sikushtuka sana, nikawaambia wakamwangalie kwa rafiki yake, Raphael, wakasema hata huko nako, Raphael mwenyewe haonekani kwao!”

IMG_9961Mama Raphael

MSHTUKO WA KWANZA

“Ukweli nilishtuka kusikia hivyo, hasa kutokana na umri wao, hivyo niliporudi nyumbani nikaendelea kuhakikishiwa kuwa, watoto wote hawaonekani. Nilichanganyikiwa, nikakosa nguvu! Yaani watoto wapotee kambini tena kambi ya polisi, sikupata jibu!”

WAINGIA MTAANI KUWASAKA

“Ilibidi tuingie mitaani kuwatafuta kila kona, tulitumia pesa nyingi mimi na mwenzangu, baba wa Raphael (Sammy) lakini bila mafanikio. Tuliposikia kuna mtoto ameonekana Mkuranga (Pwani) tulikwenda, sijui wapi, tulikwenda. Hiyo ni Oktoba mwaka jana.”

watoto wanyongwa (4)

WAKATA TAMAA

“Ilifika mahali tuliamua kumwachia Mungu kwamba yeye ndiye anajua yote, maana hakukuwa na hata tetesi kwamba wapo sehemu fulani. Tukawa tunaishi tukisikilizia kwamba watapatikana au watatokea na kusema walikuwa wapi.”

MEI 27, MWAKA HUU

“Ilipofika Mei 27, mwaka huu sasa tukiwa bado na matumaini ya kuwaona watoto wetu wakiwa hai, mimi nilipigiwa simu na mtu mmoja na kuambiwa kuna mabaki ya miili ya watoto wawili yamekutwa kwenye mfuko wa Rambo maeneo ya Barabara ya Mwakalinga. Lakini imechukuliwa na polisi.

“Tulijua kama ni polisi watakuwa wa Kituo cha  Chang’ombe, hivyo tulifunga safari kwenda ili tukapate maelekezo. Kufika tukaambiwa wamepeleka Hospitali ya Temeke. Tukaenda huko, kufika tulitambua baada ya kuoneshwa nguo ambazo walivaa  wapendwa watoto wetu, kwamba ndiyo hizohizo walizovaa siku walipotoweka nyumbani. Basi, ndiyo tukaichukua na kuandaa mazishi. Kwa kweli imetuuma sana sisi kama wazazi,” alisema mzazi huyo.

MAMA MZAZI NAYE ANENA LA MACHOZI

Naye mama mzazi wa mtoto Raphael, Lucy Fridorin (34) yeye alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kutotoa ushirikiano wa kutosha kuwatafuta watoto hao.

“Nazungumza kutoka moyoni, tangu wamepotea watoto wetu jeshi la polisi na viongozi wetu hapa kambini hawakuonesha ushirikiano wa kutosha kuwatafuta watoto wetu.

“Yaani inauma sana, watoto wapotee kambini! Ikiwa tumepotelewa sisi askari wenye jukumu la kulinda amani ya nchi je, wakipotelewa raia wa kawaida inakuaje?”

KILIITISHWA KIKAO

“Baada ya watoto kupotea, kiliitishwa kikao mara moja tu tena baada ya miezi miwili kupita kuelezea juu ya kupotea kwa watoto wetu lakini halikuongelewa lolote lile la maana,” alisema kwa uchungu mwanamke huyo huku akimwaga machozi.

Naye mama Julius, Modesta (40) pia alilitupia lawama jeshi hilo kwa kutokufanya juhudi za kutosha kuwatafuta watoto wao hadi ipookotwa miili yao baada ya miezi nane.

ANACHOJUA KAMANDA WA POLISI

Baada ya maelezo hayo, Uwazi lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ACP Gilles Mroto ambapo alisema:

“Sisi kama polisi tunachojua wale watoto waliuawa, iwe walinyongwa walifanywa nini, lakini jibu la mwisho waliuawa na tunafanya uchunguzi.”

Marehemu hao walizikwa Mei, 30 mwaka huu, kwenye Makaburi ya Kanisa la Anglikana Buza, Dar. Mungu azilaze pema peponi roho zao. Amina.

Leave A Reply