The House of Favourite Newspapers

Nani ana wajibu wa kujishusha, mwanamke au Mwanaume?

0

marriage-rocks_2523272bMUNGU ni mwema kila wakati. Tumshukuru yeye kwa kutupa pumzi na kuweza kutukutanisha tena katika safu hii ya Love Story. Tunajifunza, tunaelimika na hakika niwashukuru wale wote ambao wananitumia ujumbe mfupi kuonesha wanaguswa na kile ninachokiandika kila wiki kwenye safu hii.

Wiki hii tunayo mada iliyopo hapo juu. Kizazi cha sasa kinajikuta kwenye matatizo makubwa ya migogoro ya ndoa kutokana na maendeleo au kuiga tamaduni za magharibi.

Wanawake wanasema haki sawa. Tafsiri wanayojenga kichwani ni kwamba, hawakubaliani na mfumo wa mwanaume kuwa kichwa cha familia.

Wanataka kuona kunakuwa na usawa katika kila jambo. Wanataka kama suala la kazi, wote wawe wanafanya bila upendeleo kwamba kazi hizi ni za wanaume. Hakuna kuzidiwa, mama anafanya kazi zote zinazofanywa na baba. Eti awe analipwa sawasawa na baba anavyolipwa.

Wanataka pale nyumbani, wawe na maamuzi na sauti sawa. Kinachoweza kuamuliwa na baba basi pia kiamuliwe na mama. Wanataka kuona hakuna mkubwa katika familia. Mama na baba wote wawe na maamuzi na mamlaka sawa katika familia.

Ndugu zangu, kuna kila sababu ya kufahamu kwamba kuna uhalisia ambao upo kwamba pamoja na usawa huo wanaoupigania wanawake, mwanaume atabaki kuwa mwanaume tu.

Sina maana kwamba nachochea mfumo dume, lakini kwa mpango wake Mungu, tunatambua kuwa mwanaume ndiyo kichwa cha familia.

Love couple flirting and hugging in bedHiyo ni asili yetu wanadamu hata tukiikataa, haina maana. Kila mtu anajua, unakuta baba na mama wanafanya kazi lakini pasipo shinikizo lolote, siku zote baba ndiye anayebeba jukumu la kuihudumia familia.

Watoto wanataka ada ya shule, chakula kimepungua ndani, mavazi na mambo mengine mengi, baba lazima ajitutumuwe, atekeleze.

Baba atahudumia kwa sababu anatambua ni jukumu lake. Si tu kwa uhalisia wa kibinadamu lakini pia anatimiza matakwa ya maandiko matakatifu. Hebu tujifunze kidogo. Biblia takatifu kupitia Kitabu cha Mwanzo, sura ya 3:19 inasema; Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.’’

Kula kwa jasho kwa mwanaume ilikuwa ni laana au matokeo ya adhabu ya Mungu kwa wanaume wote kupitia kwa Adam ambaye tunaamini ndiye binadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu, alipokubali kudanganywa na Eva.

Eva alidanganywa na nyoka, akala lile tunda ambalo Mungu aliwakataza. Mungu akamlaani nyoka, akamlaani mwanamke sambamba na mwanaume pia.

Nyoka aliambiwa, nanukuu Mwanzo 3: 14-15: Hivyo Bwana Mungu akamwambia nyoka, ‘‘kwa kuwa umefanya hili, ‘‘Umelaaniwa kuliko wanyama wote wa kufugwa na wa porini! Utatambaa kwa tumbo lako na kula mavumbi siku zote za maisha yako. Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, atakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino.’’

Tangu hapo tumeona hiyo ndiyo ilikuwa laana kwa nyoka. Anatembea kwa tumbo lake na kula mavumbi na kweli ni adui wa mwanadamu.
Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi.

Leave A Reply