The House of Favourite Newspapers

Nape Nauye: Lady Jaydee Ameuheshimisha Muziki wa Tanzania – Video

Mbunge wa Mtama, Nape Nauye

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amempongeza msanii mkongwe Lady Jaydee kwa mchango wake mkubwa katika kukuza na kuiheshimisha sanaa ya muziki wa Tanzania.

Akizungumza katika usiku wa sherehe ya kuadhimisha miaka 25 ya mwanamuziki huyo kwenye tasnia ya muziki, iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki – Dar es Salaam, Nape amesema kuwa Lady Jaydee ni miongoni mwa wasanii walioweka historia isiyofutika katika muziki wa Bongo Fleva.

Msanii mkongwe Lady Jaydee

“Lady Jaydee si tu msanii, bali ni alama ya muziki wa Tanzania. Ameuheshimisha muziki wetu na kutufikisha mbali kimataifa,” alisema Nape.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo wasanii wenzake, wanasiasa, na mashabiki waliokuja kumpongeza kwa safari yake ya nusu karne katika sanaa.