The House of Favourite Newspapers
gunners X

Nape Uwe Kamanda, Tuwabebe Serengeti Boys

MAKALA: Saleh All | CHAMPIONI | Dar es Salaam

BAADA ya timu ya taifa ya vijana chi­ni ya miaka 17, Serengeti Boys kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Af­con), kinachoanza sasa ni maandalizi.

Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kambi itakuwa nje ya nchi kwa ajili ya kuhakikisha in­akuwa katika maandalizi bora.

Tunakumbuka timu hiyo iliwahi kuweka kambi nje ya Tanzania, ilikuwa nchini Madagascar na vija­na wakajiandaa na kufani­kiwa kufuzu.

Wako ambao wame­kuwa wakiamini Serengeti Boys kama imesaidiwa, lakini ukweli ni kwamba Congo Brazzaville waliwe­ka dhuluma lakini mwisho haki imepatikana na vijana wamefuzu na kuingia kwenye hatua wakliyosta­hili.

Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Mich­ezo, Nape Nnauye amekuwa waziri wa kwanza anayehusi­ana na michezo kuwa active, yaani anayewe­za kuendana na kasi ya michezo.

Michezo ina kasi kubwa katika kila nyanja. Unawe­za kuona ajabu, lakini uk­weli yule anayehusika na michezo anatakiwa kuwa mwepesi na mwenye maamuzi ya haraka . Mara nyingi wanaofanya shu­ghuli za michezo wamekuwa wepesi katika utekelezaji.

Mawaziri wengi walishindwa kwenda na kasi ya michezo, to­fauti na Nape ambaye ame­onyesha mfano mkubwa na unaweza kusema hatua zake zimekuwa ni za har­akaharaka sana na mam­bo mengi ameyafanya kwa muda mfupi.

Leo nimeandika kueleza namna ambavyo nimeona Nape akishiriki katika mich­ezo na hasa kuhusiana na kusaidia mambo kadhaa bila ya kujitokeza.

Mfano nini kifanyike kwa vijana hao, kuwaomba watu wajitokeze kuwasaidia na kadhalika. Jambo ambalo ninaipongeza serikali kupitia Nape kwamba wameonyesha kuwajali vijana ambao nao wamewalipa.

Lakini naona huu ndiyo wakati mzuri wa serikali kusi­mama tena si ikibaki chini na kusukuma. Badala yake itan­gulie mbele na ikiwezekana suala la Serengeti Boys liwe la kitaifa na kwa pamoja tuisaidie hii timu ya vijana.

Kama unakumbuka, juzi nilil­ishauri Shirikisho la Soka Tan­zania (TFF) kuweka hadharani kwamba wana kiasi gani, kiwe cha msaada au walichokusanya na baada ya hapo watueleze wadau wamepungukiwa kiasi gani badala ya kusimama had­harani na kusema Sh bilioni moja pekee ndiyo inatakiwa.

Nilitaka vitu vingi viwe vya uwazi huku nikikumbusha kuondoa suala la hofu. Kwa kuwa kuna fedha nyingi za wad­hamini au wafadhili na kume­kuwa na hali ya hofu baada ya kuwa tumeelezwa mahesabu yana walakini na kadhalika.

Katika hili la kuichangia Ser­engeti Boys lazima kuwe na umakini yakinifu kwa kuwa kama serikali itawaacha TFF peke yao na hapa tunazun­gumzia michango, basi huenda hofu ikachangia wengi wa­sichange.

Kama hakutakuwa na michango ya kutosha kutokana na hofu, basi wengi tutaiangu­sha Serengeti Boys ambayo ni timu mali yetu na wala si ya TFF.

Ndiyo maana nimeamua kuweka msisitizo na kuiomba serikali isimame imara tena mstari wa mbele na ikiwezeka­na Nape awe mwenyewe ili wadau waingie msituni kusaka michango na kuwashawishi kuichangia timu yetu.

Suala la serikali kuipigania Serengeti Boys haliwezi kuwa geni. Kweli imefanya lakini mimi naona bado haitoshi na juhudi kuu zinahitajika kuhakikisha vi­jana wanakwenda wakiwa na ari ya juu zaidi na ikiwezekana walionuia kufanya vizuri.

Wanapokwenda ni pagumu kuliko walipotoka kwa kuwa bora ndiyo wanakwenda kuku­tana huko. Hivyo watakutana na walio bora kuliko waliowafunga au kuwavuka. Hii haitakuwa kazi rahisi kwa vijana hawa.

Tukubali wanahitaji msaada mkubwa kuliko wa awali, wana­hitaji kuhudumiwa na kuanda­liwa kwa kiwango cha juu kuliko ilivyokuwa awali. Na serikali ikiamua, kamwe haitashindwa kutekeleza hilo na vijana wetu wakaenda Afcon wakiwa na ari ya juu.

Hawa vijana ndiyo nguzo au gia ya mabadiliko ya mch­ezo wa soka nchini. Hawa ndiyo mashujaa wetu wa baadaye na watatuondoa hapa topeni tu­lipokwama.

Hivyo namshauri Nape asi­mame mbele kama kamanda, tuwapiganie vijana na wadogo zetu tukiamini wakihamasika, watafanya vizuri kwa kuwa tayari wametuonyesha ni watu wenye kunuia na wanatekeleza lakini watakuwa mabadiliko ya mchezo huo hapa nyumbani hapo baadaye.

Comments are closed.