The House of Favourite Newspapers

Nas B: Bongo Fleva Inatumbukia Shimoni

0
Nas B.

MKALI wa muziki Bongo aliyewahi kutamba na Ngoma za Kawaida, Dua la Kuku na Tunatumia ambaye pia ni Prodyuza wa Pamoja Records, Nas B amefungukia Muziki wa Bongo Fleva kuwa unaelekea shimoni kwa sababu wasanii wengi wanaamini mafanikio yapo mitandaoni kuliko redioni na kwenye TV.

Akichonga na Showbiz ya Gazeti la Ijumaa, Nas B alisema kuwa, wasanii wengi wanajitutumua kufanya muziki mzuri lakini mwisho wa siku unaishia mitandaoni, jambo linalochochea kuua muziki huo.

“Nimefanya sana muziki ikiwa ni pamoja na kuutengeneza, nimeshawate-ngenezea mastaa kibao lakini nionavyo mimi muziki wetu kama unaelekea shimoni, msanii yupo tayari kuingia studio kurekodi video na audio kisha zinaishia mitandaoni akiamini ndipo kwenye mafanikio,” alisema Nas B ambaye anasimamiwa kwa sasa na Meneja Chief.

Leave A Reply