The House of Favourite Newspapers

‘Nateseka na Wadudu Miguuni’

0

MGUU VIDUDU (3)Gerald Mwambungu.

Stori: Mayasa Mariwata na Gabriel Ng’osha

KWELI hujafa hujaumbika! Kijana Gerald Mwambungu (33), mkazi wa Ubungo Dar, alizaliwa akiwa mzima lakini akaja kupatwa na tatizo la wadudu miguuni ambao wamekuwa wakimsababishia maumivu makali na baadaye ulemavu.

MGUU VIDUDU (2)Miguu ilivyoshambuliwa na wadudu

Akizungumza kwa majonzi na Uwazi hivi karibuni, Mwambungu alisema tatizo hilo lilimuanza mwaka 2014 baada ya kutokwa na kipele kwenye mguu wa kulia ambapo alihisi kuwashwa na kulazimika kujikuna mara kwa mara na kupasuka baada ya siku mbili.

“Sasa kilivyopasuka nikashangaa badala ya kidonda kupona, kikawa kinasambaa siku hadi siku.

MGUU VIDUDU (1)AENDA HOSPITALI

“Nilikwenda Hospitali ya Amana (Dar) wakakisafisha kidonda lakini wakaniambia wameshindwa, niende Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Pale kidonda kikasafishwa na kupewa dawa. Baada ya wiki moja kikaonekana kupona, lakini siku chache mbele nikaanza kuona vitu vya ajabu kwenye ngozi. Hapo sasa nikawa nashindwa kutembea sawasawa kama unavyoniona. Nilipokwenda tena hospitalini, wakanifanyia vipimo na kugundua ndani ya mguu kuna wadudu. Napata maumivu sana jamani!

MGUU MWINGINE WADAKIA

“Nikiwa kwenye tiba,  mguu wa kushoto nao ukadakia, ukawa na wadudu,” alisema Mwambungu.

INDIA NDIYO KUNA TIBA

“Madaktari waliniambia tatizo la miguu yangu kuwa na wadudu lazima niende nchini India kutibiwa na wakasema gharama ni shilingi milioni 15. Walisema hapa Tanzania tatizo langu limeshindikana na ugonjwa umeshaenea mwili mzima. Na ni kweli maana hawa wadudu kama unavyoona ni mwili mzima.”

NI UGONJWA GANI?

Katika mahojiano maalumu na Uwazi, daktari mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema dalili alizonazo Gerald, zinafanana na za ugonjwa wa Lymphatic Filariasis (LF) ambalo husababishwa na kung’atwa na mbu wenye vimelea vya Filaria ambavyo vikiingia ndani ya mwili wa binadamu, hubadilika na kuwa wadudu (microfilariae) ambao hujirundika ndani ya ngozi na kuendelea kuzaliana kwa kasi.

HANA NDUGU DAR

“Hapa Dar mimi sina ndugu, nilikuja kutafuta maisha nikitokea wilayani Kyela (Mbeya) miaka miwili iliyopita. Nikaanza kuuza viatu vya mitumba Ubungo na sina makazi ya kueleweka. Hapa nipo kwa rafiki yangu kanisitiri,” aliongeza.

Aliyeguswa na tatizo la Mwambungu anaweza kumsaidia kwa namba; 0716 631148, 0767 362146 na akaunti namba CRDB 0152451074900.

Leave A Reply