The House of Favourite Newspapers

Nature: Singeli Haiwezi ‘Kufa’



STORI: NA ANDREW CARLOS | AMANIShowbiz Xtra

MKONGWE wa Muziki wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’ amefungukia baadhi ya madai ya watu wanaosema Muziki wa Singeli ni wa muda mfupi na kuwaambia kuwa, hata iweje muziki huo hauwezi kupotea ‘kufa’ kwani umekaa kiasili.

Nature anayebamba na Ngoma ya Mtumba aliiambia Showbiz Xtra kuwa, muziki huo unakubalika kwa kila rika na umeweza kuchuana na Bongo Fleva.

“Ni muziki ambao umepokelewa vizuri na unakubalika, ukitaka kujua unakubalika vipi tembelea uswazi ujionee. Binafsi hauwezi kufa kwani una vigezo vyote vinavyoufanya uendelee kuwa hai,” alisema Nature.

Nature anatarajiwa kuungana na wakali wa Singeli Sikukuu ya Pasaka ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar ambao ni Msagasumu anayetikisa na Ngoma ya Matobo pamoja na Dulla Makabila anayetikisa na Utatoa Hutoi.

Akizungumzia sikukuu hiyo, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema mbali na uwepo wa Nature, Msagasumu na Dulla Makabila, jukwaa litavamiwa na msanii ambaye ni gumzo kwa sasa Harmorapa.

“Tutakuwa pia na Khadija Kopa akiwa na bendi yake ya Taarab ya T.O.T, Mshindi wa Wikienda Music Search (WSM), Frank Melodies na Babu Elly na pambano la ngumi la kukata na shoka,” alisema Mbizo.

Comments are closed.