The House of Favourite Newspapers

Nay: Shilole Atafunika Usiku wa Wapo Dar Live

0

Stori: NA MWANDISHI WETU | RISASI | Risasi Vibes

STAA wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anatarajiwa kuungana na msanii mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ katika bonge la shoo lijulikanalo kama Usiku wa Wapo, Mei 20, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Vibes, Nay alisema kuwa, baada ya kusikia kilio cha mashabiki wengi wa muziki wake wakimtaka kuipeleka Wapo Dar Live sasa yupo tayari kukata kiu yao.

“Watu wangu wa Mbagala,Temeke, Tandika, na Dar es Salaam kwa ujumla kilio chenu nimekisikia na Wapo kwa mara ya kwanza itashushwa ndani ya kiwanja chako cha Dar Live nikiwa na mwanangu Shilole niamini mimi, Shilole siku hiyo atafunika vilivyo.

Shilole

“Listi kamili bado inakujia hivyo ni wakati wako kutega sikio na kusoma Magazeti ya Global kujua zaidi,” alisema Nay.

Shoo ya Usiku wa Wapo itasindikizwa na Mshindi wa Ijumaa Wikienda Music Search (WMS), Mgogosi Melody.

Kabla ya shoo hiyo, Mei 13 kunatarajiwa kuwa na shoo ya nguvu katika kiwanja hicho kutoka kwa kundi kongwe la Muziki wa Taarab, Jahaz Modern.

 

Tazama Nay wa Mitego Akiimba Live Wimbo Wake Wapo

Leave A Reply